MATANGAZO YA BIASHARA.(Advertisement sites)
Nini maana ya kutangaza?
Ni kitendo cha kuvuta makini ya umma kwenye biashara kwa lengo la kuuza bidhaa au huduma kwa kutumia njia mbalimbali kama magazeti, mitandao ya kijamii, mbao za matangazo n.k.
Matangazo ndio njia ya Mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mtoa huduma na mteja na mteja mtarajiwa.
"Biashara ni matangazo" na Biashara ni watu. Na hao watu lazima watambue biashara yako na bidhaa unayouza. Na njia pekee ya kutambulisha biashara yako ni kupitia matangazo.
LENGO LA KUTANGAZA BIASHARA:
1. Kufanya wateja wako kutambua bidhaa au huduma unayotoa.
2. Kuwashawishi wateja wako kuwa bidhaa au huduma yako ni sahihi kwa mahitaji yao.
3. Kutengeneza mvuto kwenye bidhaa yako au huduma yako.
4. Kuonesha mfumo taswira au muundo wa biashara yako.
5. Kutangaza bidhaa mpya au huduma mpya unayotoa.
6. Kukazia ujumbe au taarifa kwa wauzaji na wanunuzi.
7. Humfanya mteja kuchukua hatua zaidi ( kuuliza taarifa kama vile, mfano wa bidhaa, mahali zinapipatikana, namna ya kuagiza, namna ya kuzipata n.k.)
8. Kuwavuta wateja kwenye biashara yako.
Kama ulifuatilia taa zilizotangulia utakumbuka tuliongelea Umuhimu wa mpango biashara kwa mjasiriamali, Mpango biashara ndio hutoa taswira ya biashara yako. Malengo mahususi ya biashara ni lazima yawe yameainishwa katika mpango biashara (business plan). Kwa mfano: katika mpango biashara utakuwa umeainisha namna biashara yako itakavyokuwa inakua, namna utakavyofanya mauzo ya bidhaa yako na kwa asilimia ngapi itapata faida.
Matokeo unayoyatatajia katika biashara yako ndiyo yatakayoonyesha ni kwa jinsi gani urekebishe mfumo wa biashara yako. Ikiwa unatarajia matokeo makubwa katika biashara yako ni lazima utengeneze mifumo mathubuti itakayokuwezesha kufikia matokeo hayo katika biashara yako. Malengo na matarajio hutegemea sana soko ulilomo na uzalishaji wako.
> Bidhaa na biashara zote ni lazima zipitie hatua tatu, Zote zikiwa na malengo ya kujitangaza:-
1. Biashara Inayoanza ( the start-up business).
Wewe ni mpya kabisa katika soko na unahitaji kujipambanua upekee wako ili ujulikane! Utahitajika kufanya matangazo kwa ubora, kwa nguvu na kwa kiwango cha juu pamoja na kutoa ofa zitakazofanya uteke makini ya wateja wako na kutambua uwepo wako sokoni.
2. Biashara inayokua (the growing business).
Baada ya kutambulika kwa wateja kitu kinachotakiwa ni kujitofautisha na washindani wako ili uweze kuwashawishi wateja kujaribu bidhaa au huduma yako. Mteja huanza kwa kujaribu na akivutia hugeuka kuwa mteja wa kudumu kabisa na kukusaidia kutangaza kwa wengine pia kutokana na ubora wa bidhaa au huduma yako.
3. Biashara iliyoimarika (the established business).
Katika hatua hii biashara inakuwa imeanza kusimama na lengo la kufanya matangazo ni kuendekea kumkumbusha mteja wako kwamba ni kwa nini aendelee kutumia bidhaa au hiduma yako.
Haijalishi biashara yako ipo katika hatua gani, mteja hupitia hatua nne kabla hajawa mteja wa kudumu. Nawewe unapotangaza biashara yako hakikisha unampitisha katika hatua hizo.
Hatua hizo zinaweza kufupishwa kwa kiingereza kwa neno "AIDA"
A- AWARENES
Mteja ni lazima atambue huduma au bidhaa unayotoa.
I- INTEREST
Ni lazima uteke kile ambacho mteja anakipenda na umwambie kuwa bidhaa yako itawasaidiaje au itawafanyia nini!
D- DESIRE
Hakikisha mteja anatamani kujaribu kutumia bidhaa au huduma yako.
A- ACTION
Baada ya kuvutiwa na kutamani mteja atachukua hatua ya kuuliza kupata taarifa zaidi kuhusu bidhaa au huduma na hata kuamua kununua bidhaa yako.
Hatua za kuzingatia unapokuwa unafanya matangazo.
1. Tambua soko lako.
Ni lazima utambue kundi la watu ambao bidhaa yako inawalenga ( Ni kundi lipi ambalo linapendelea kununua bidhaa yako?) Ukishatambua wateja wako ni lazima pia ujitahidi kujua hata maeneo ambapo wanapatikana mara kwa mara na kwa wingi. Mfano! Unatangaza biashara ya nguo na vifaa vya michezo, wateja wako wengi ni vijana na wapenda michezo, kwa hiyo ukiweka tangazo lako kwenye gazeti la "Mwanasport" utawapata wengi.
2. Tengeneza bajeti yako.
Baada ya kujua walengwa wa huduma yako, hatua inayofuata na kuandaa bajeti ya namna na gharama utakazotumia kuwafikia walegwa.
3. Panga ni njia gani utaitumia. Baada ya kuwabaini wateja wako na kiasi cha fedha unachokusudia kukitumia kwa matangazo tafuta sasa njia itakayowafikia walengwa wako kwa kuzingatia bajeti yako.
4. Tengeneza mkakati wa matangazo yako.
Tafuta ujumbe ambao unavutia na utakaofanya tangazo lako lifike kwa wahusika, kama ni picha, sauti au video ziwe za kuvutia na zinazoendana na kile unachotangaza na kundi la wateja unaolenga.
SIFA ZA TANGAZO LINALOFAA KWA BIASHARA.
Haijalishi aina ya biashara unayofanya lakini kuwa na mpango wa biashara ni kitu cha muhimu sana.
Ikiwa utashindwa kuitangaza biashara yako kwa ufasaha itakuwa ni vigumu sana biashara yakokufanikiwa. Hivyo basi ufahamu juu ya sifa za tangazo bora la biashara kutakusaidia sana kuweza kupanga biashala yako vizuri
> Zifuatazo ni sifa za tangazo bora:-
1. Rahisi kukumbukwa.
Ili tangazo liwwze kuwa na ufanisi kwa msomaji ni lazima liwa linakumbukika kwa urahisi kwa msomaji, msikilizaji au mtazamaji
Kwa tangazo tenye ufanisi mtazamaji lazima aweze kurejea kwa urahisi kile kilichotolea kwenye tangazo na muhimu zaidi ni lazima akumbuke ni bidhaa gani iliyokuwa inatangazwa kwenye tangazo. Kukumbukwa ndicho kitovu cha tangazo bora.
2. Ni lazima Liwalenge wahusika (wateja) kwa ufanisi.
Sehemu ngumu katika kutengeneza na kuendesha matangazo ya biashara ni kujua walengwa wa biashara, hakuna biashara ambayo inanlenga kila mtu kwa asilimia zote. Kwa hiyo ni muhimu kujua sehemu ya jamii ya watu utakaowahudumia ili kuepusha kupoteza muda na pesa kuwatangazia watu ambao sio walengwa. Kwa kutambua hivyo itakusaidia kufanya maamuzi ya aina ya njia ya matangazo utakayotumia. Kama utatumia Tv utatumia kituo kipi ambacho unafikiri wateja wako hupatikana mara nyingi na kwa wingi.
3. Ni lazima liwe linaburudisha.
Tangazo lenye ufanisi linatoa taarifa ya bidhaa au humuma kwa mteja, lakini hiyo haitoshi kama halitamburudisha mteja na kumvutia kuliona au kulisikia tena na tena. Kuteka makini ya mtumiaji ni muhimu kwa mtangazaji, na hivyo kwa kadri utakavyomburudisha zaidi ndivyo utakavyofanikisha kuteka makini ya mtumiaji. Kama inakubalika ni vizuri kuhusisha kitu kinachochekesha kidogo katika tangazo, hii itakusaidia kuteka makini ya mtumuaji.
4. Kuteka makini ya mtazamaji au msikilizaji.
Uzuri wa tangazo si chochote kama tamgazo halitaonekana kwa watu. Kitu muhimu katika tangazo ni kuhusisha kitu ambacho watu wako wanakipenda na kinachovuta umakini wao zaidi. Kwa hiyo kwa vile ni muhimu kuvuta umakini wa wateja husika Ni muhimu kujaribia miundo mbalimbali ya matangazo na kisha inachagua ile inayovitia zaidi.
Vitu ambavyo watu wanakosea katika matangazo ya biashara.
1. Kuelezea huduma au bidhaa badala ya kueleza kile ambacho mteja atafaidika na huduma au bidhaa yako. Isikazie tu kueleza uzuri wa biashara yako badala ya kuelezea manufaa ya bidhaa au huduma kwa mtumiaji.
2. Kuelezea bidhaa zaidi badala ya Kuelezea yule anayetoa huduma au bidhaa.
Mtumiaji anatamani zaidi kumfahamu yule anayetoa bidhaa au huduma na baada ya kumwamini ndipo ataweza kutoa pesa yake.
Makampuni makubwa yanayouza sana bidhaa siyo kwamba bidhaa ndiyo inafahamika sana bali jina la kampuni au mmiliki wa kampuni ndiyo linaaminika.
Kama wewe ni mwalimu jitahidi kuwafanya wateja wako wakufahamu wewe zaidi siyo kuifahamu shule au tuisheni yako zaidi hiku wewe ukijificha nyuma ya majengo na mavitabu.
3. Kuweka tangazo sehemu isiyohusika. Siyo kila mahali penye watu wengi panafaa kuweka tangazo japokuwa tangazo inabidi lionekane na watu wengi. Unaweza ukawa umeweka matangazo sehemu ambapo watu wapo bize sana, hivyo si rahisi kupoteza muda kuangalia tangazo. Au unaweza kuweka tangazo ambapo watu wanakuja kwa kusidi lingine. Mfano facebook, instagram n.k watu huja kwa ajili ya kujiburudisha na mara nyingi huja wakiwa wamechoka wala hawaji kutafuta bidhaa. Kufanya hivyo ni sawa na kutangaza biashara kijiweni ambapo watu wapo kupiga stori zao. Utakuwa unawakera na wala hawatakusikiliza ni bora ukamuita mtu pembeni na kumshirikisha bidhaa au huduma unayotoa.
**** Kitu unachoweza kukifanya ni kuwahamisha watu kutoka huko na kuwaleta sehemu ambapo utawapatia tangazo hilo kwa ufasaha zaidi.
** Hivyo unaweza kutumia mitandao ya kijamii kama sehemu ambayo utawakusanya watu ili uweze kuwatangazi bidhaa na wala siyo sehemu ya kutangazia.
Mfano: Unaweza kuwavuta wahatsApp inbox, Kwenye Email, blog, website n.k hapo wataweza kuliza na kupata maelezo zaidi kuhusu wewe na bidhaa yako.
0 maoni: